Wednesday, 10 January 2018

okwi hadai chochote simba

Ni muda sasa umepita bila Okwi kuonekana kwenye kikosi cha Simba, taarifa zinaeleza kwamba mchezaji huyo yupo nchini kwao akiendelea na matibabu baada ya kuumia shingo.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Hans Poppe amesema taarifa alizonazo ni kwamba, nyota huyo aliyesajiliwa msimu huu bado anaendelea na matibu na si vinginevyo kama baadhi ya watu wanavyosema kuwa anadai pesa zake za usajili.

“Nilivyopata habari Okwi ni kwamba alikuwa bado anauguza shingo huko kwao sasa kama hayupo ni kwa sababu ya kuumwa”-Hans Poppe.

“Kama kuna maneno mengine zaidi ya hayo sidhani kama ni kweli kwa sababu ni mchezaji ambaye hadai kitu chocchote alipata malipo yake yote, wachezaji wote hakuna ambao wanadai kwamba afanye kwa makusudi kwa sababu hajalipwa haki zake.”

Siku za karibuni iliripotiwa kwamba, Okwi ametia mgomo kwa sababu anadai pesa za usajili ambazo hajalipwa, hivyo kukaa kwake Uganda ni kushinikiza uongozi wa klabu hiyo umalizie kiasi anachodai

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...