Jeneza lenye mwili wa marehemu Makaidi likiwa mbele wakati ibada maalum ya kumuombea ikiendelea.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wakiwa wamekusanyika Viwanja vya Karimjee kuuaga mwili wa mpendwa wao, Dk Makaidi.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema akiwakilisha Ukawa, Edward Lowassa akipita kuaga mwili wa marehemu Makaidi.
Jeneza likiwa juu ya kaburi, viongozi wa Ukawa wakiwa wameketi wakati wa maombi maalumu kabla ya mazishi kuanza.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Makaidi likiwa limewekwa juu ya kaburi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Dk Makaidi likiingizwa kaburini.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Dk Makaidi likiingizwa kaburini.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema akiwakilisha Ukawa, Edward Lowassa amewaongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NLD ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Dk. Emmanuel Makaidi katika Viwanja vya Karimjee na kuzikwa katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Baada ya mwili wa marehemu kuagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ulipelekwa moja kwa moja kupumzishwa katika nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya Sinza, Dar.
Marehemu Dk. Makaidi alikutwa na mauti Oktoba 15, mwaka huu akiwa mkoani Lindi kwa shinikizo la damu na alikuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Masasi.
PICHA NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment