Tuesday, 10 October 2017

Taifa dogo kabisa Duniani kufuzu kombe la Dunia likiwa na idadi ya watu, 335,000

Gylfi Sigurdsson celebrates after his goal put Iceland into the lead against KosovoGylfi Sigurdsson akishangilia goli la ushindi kwa nchi yake.
Iceland imekuwa nchi ndogo zaidi kuwahi kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kuwalaza Kosovo 2-0 na kumaliza kileleni kundi lao la kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Urusi 2018.
Iceland, ambao walifika robofainali Euro 2016, baada ya kuwaondoa England hatua ya 16 bora, ni taifa la raia 335,000 pekee.
Ndiyo nchi ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia ikiwa na idadi ya watu ambao ni chini ya milioni moja.
Gylfi Sigurdsson wa Everton na Johann Gudmundsson wa Burnley ndio waliofungia taifa hilo Jumatatu.
Sigurdsson aliwapa matumaini kwa kufunga muda mfupi kabla ya mapumziko na kisa akamsaidia Gudmundsson kufunga bao la kuwahakikishia ushindi.
Iceland sasa wameshinda mechi saba kati ya 10 Kundi I la kufuzu kwa Kombe la Dunia.

The Everton midfielder put his country in front on 40 minutes - to the delight of his team-matesMshambuliaji wa klabu ya Everton akishangilia goli lake la ushindi aliloifungia klabu yake.

Iceland's euphoric squad celebrate in front of their fans during a memorable night in Reykjavikkikosi cha timu ya Taifa ya ICELAND ikishangilia kuingia katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 URUSI
MATAIFA MADOGO DUNIANI
World Cup minnows

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...