Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk
Albina Chuwa ametoa takwimu hizo leo Desemba 1 katika maadhimisho ya siku ya
Ukimwi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Dk Chuwa amesema mkoa wa Lindi umekuwa wa mwisho kwa watu
wenye virusi vya ukimwi na idadi ya asilimia 0.1 huku maambukizo kwa Jiji la Dar es Salaam
yamepungua hadi kufikia asilimia 4.7 ikiwa na maana watu 133,971 wanaishi na
ugonjwa huo.
Mkurugenzi huyo amesema kwa ujumla watu 1.4 milioni nchini
Tanzania wanaishi na virusi vya Ukimwi na takwimu hizo ndiyo rasmi hivyo
asitokee mtu au kikundi cha watu kupotosha.
"Nasema kwa sababu kuna watu wanakurupuka na kuja na
takwimu zao. Naomba watambue takwimu ni fani kama fani nyingine na zina miiko
yake," amesema Dk Chuwa
Hata hivyo, Dk Chuwa amesema Serikali haimzuii mtu au
kikundi kufanya utafiti ila ni lazima awasiliane na ofisi ya takwimu wapitie
dodoso zake kabla ya kuruhusiwa kufanya.
Amesema atakayekiuka na kupotosha takwimu adhabu yake
iliyowekwa kisheria ni kifungo cha miaka mitatu au faini Sh10 milioni au vyote
kwa pamoja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na
virusi vya Ukimwi, Justin Mwinuka ameiomba Serikali kutengeneza Sheria
zitakazoratibu upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya ukimwi (ARV).
Mwinuka amesema uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuwabana watu
wanaofanya biashara kupitia dawa hizo.Amesema wagonjwa wengi hawapati dawa
kutokana na kushindwa kumudu gharama.
"Tuna changamoto ya uhaba wa dawa na zinazopatikana
zinauzwa sasa wagonjwa wanashindwa kupata fedha za kununua,"
No comments:
Post a Comment