jina kamili :
Ernesto Guevara
Kazi :
Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)
Uraia :
Argentina
Kuzaliwa :
June 14 1928
Kufariki :
October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera
Chanzo cha
kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi
Kama kijana
msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara
la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona
maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko
mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo
kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.
Miaka ya 50
akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na
Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba
wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na
America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na
kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada
ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika
serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu
ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama
waziri wa kilimo wa Cuba.
Mwaka 1964
akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New
York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa”
pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo
juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa
akisema
“wale wanaoua
watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu
wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na
mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao,
vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”
MGOGORO WA
CONGO – DRC
Miezi michache
baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life”
na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa
akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi
ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na
akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar
es salaam huku akiishi kwa kujificha
Baadae mwaka
1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia
kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye
makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana
baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka
kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya
montane dry fores
KUKAMTWA NA
KUUWAWA
Mwaka 1967,
makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix
Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia,
asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo
yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa
kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,
Yasemekana
baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
“Usifyatue
risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata
nimekufa”
Alifungwa kama
na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi
wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo
huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili
hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja
kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya
kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga
risasi sita za kifua na kufa palepale
Kabla
hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja
kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”
Aliacha wake
wawili na watoto watano
No comments:
Post a Comment