Mgombea ubunge dodoma mjini Benson Kigaila Singo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA
VYOMBO VYA HABARI TAREHE 26/09/2015
Jeshi la Polisi mkoa
wa Dodoma linamshikilia Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chadema BENSON KIGAILI SINGO
na wenzake kumi (10) kwa tuhuma za KUFANYA MAANDAMANO BILA KIBALI NA KUZUIA
WATUMIAJI WENGINE wa BARABARA KUSHINDWA
KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO, KUMSHAMBULIA ASKARI,KUFANYA FUJO KITUONI NA KUTUKANA
ASKARI.
Matukio hayo
yalitokea majira ya saa 18:45 katika barabara ya Jamatini na Kituo Kikuu cha Polisi
baada ya Mgombea huyo kumaliza mkutano wake wa kampeni katika eneo la stendi
kuu ya Dodoma.
Pamoja na kupewa
maelekezo na askari kuacha maandamno hayo ili watu wengine waweze kuendelea na
shughuli zao, walikaidi na kuanza kutoa matusi na kumshambulia askari kwa chupa
ya soda jambo ambalo linaonyesha walikuwa wamedhamiria kwa sababu inakuwaje watembee na chupa tupu za soda. Na kama hiyo haitoshi
walipofika kituoni walianza kufanya fujo na kutoa matusi kwa askari.
Watuhumiwa wanaoshiliwa ni wafuatao:-
1.
BENSON
KIGAILA SINGO, MIAKA 46, Mkazi wa Ipagala/Kibakwe.
2.
KHADIJA
MAULA, MIAKA 40, MFANYABIASHARA WA NKUHUNGU
3.
STELLAH
MASSAWE, MIAKA 38, MFANYABIASHARA MKAZI WA AIRPORT
4.
GODFREY
CHARLES MANYANYA, MIAKA 29 MWENYEKITI WA VIJANA CHADEMA MKOA WA DODOMA, MKAZI
WA AREA ‘E’.
5.
HASHIMU
SELEMAN KILAINI, MIAKA 45, MFANYABIASHARA MKAZI WA AIR PORT DODOMA.
6.
ALEX
NICHOLAUS THOMAS, MIAKA 28, MFANYABISAHARA MKAZI WA CHAMWINO.
7.
PRISCA
BAKARI MGAZA, MIAKA 20, MFANYA BIASHARA MKAZI WA MAKOLE.
8.
LUCKYSON
KWEKA, MIAKA 28, MWANAFUNZI, MKAZI WA MAILI MBILI.
9.
AISHA
MAKWE URIO, MIAKA 22, MWANAFUNZI MKAZI WA AREA “D”
10.
POMPEY
MNYALAPE REMIJO, MIAKA 40, MFANYABIASHARA MKAZI WA AREA “C”.
11.
LAWI
NGA’MBIE TUMUZA, MIAKA 52, MPIGAPICHA MKAZI WA AREA “E”.
Askari
aliyeshambuliwa alipelekwa General Hospital kwa matibabu.
Nitoe wito tena kwa Wagombea
wa Vyama vyote na wananchi wa Dodoma kwa ujumla watii sheria bila shuruti kwani
umaarufu hautafutwi kwa kuvunja sheria na watambue kufanya hivyo ni kosa la
jinai. Watambue hakuna haki isiyokuwa na wajibu.
Pia wanapokwenda na
kutoka kwenye mikutano waache kufanya maandamano na hata watumiapo barabara
wazingitie sheria za usalama barabarani ili watu wengine waweze kuendelea na
shughuli zao bila bughudha au vitisho.
Aidha zipo taarifa
kuwa kuna baadhi ya Wanachama na wafuasi wa Chadema wanapita sehemu mbalimbali
wanahamasisha watu kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kushinikiza waliokamatwa
waachiliwe kabla ya taratibu za kisheria hazijakamilishwa. Watambue atakayefanya
hivyo ajue atakabiliwa vilivyo na mkono wa sheria.
Jeshi la Polisi Mkoa
wa Dodoma litaendelea kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria wale wote
watakaokiuka sheria bila kujali ana wadhifa gani.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi MISIME D.A (SACP).
source:http://mrokim.blogspot.com/2015/09/polisi-dodoma-yashikilia-10-akiwemo.html
No comments:
Post a Comment