Nape amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Njia Nne Kilwa akiwa anatoka Dar kuelekea jimboni kwake.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: "Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.
Zimeenea picha pamoja na taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu gari ya Kada wa CCM, Katibu wa Itikadi na Uenezi, na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama Mkoa wa Lindi, Nape Moses Nnauye kupata ajali… simu yake imepokelewa na Dereva wake, na hiki ndio kingine alichonifikishia kuhusu ajali aliyoipata Nape Nnauye.
“Ni kweli amepata ajali alfajiri ya leo lakini hajambo, alikuwa anaendesha mwenyewe gari… amepata ajali maeneo ya SOMANGA, barabara kuu ya kutoka Dar kwenda Lindi, ilikuwa saa 12 alfajiri..” >>> Dereva wa Nape Nnauye.
“Tulitoka Dar es Salaam saa kumi na robo tunakwenda Jimboni Lindi, alikuwa kwenye gari pekeyake mimi nilikuwa nyuma yake.. ana jeraha dogo, mkanda umemchubua mkono wa kulia kidogo… Tumetoka Hospitali, hana tatizo lolote na yuko kwenye Kikao kwa sasa“
Kuhusu hali ya gari je? >>> “Gari imeharibika sana, ni toyota Land Cruiser na iko kwenye Kituo cha Polisi Somanga“
No comments:
Post a Comment