Tuesday, 20 October 2015

makaidi kuzikwa leo katika makaburi ya sinza



Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi akiwa katika huzuni baada ya kuondokewa na mpendwa wake.

Mtoto wa kwanza wa Dk. Makaidi, Hilda Emmanuel Makaidi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
MWILI wa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi alisema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na jana jioni ulipelekwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza Vatican ambapo itafanyika ibada fupi na kupata fursa ya ndugu na majirani kuuaga.
Alisema leo mwili huo utaagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi mbalimbali wa kisiasa, serikali watakuwepo na kisha kufanyika mazishi yake katika makaburi ya Sinza.
“Unajua baba alikuwa ni mwanasiasa na amefariki akiwa bado ni mwanasiasa hivyo ni lazima uweze kuagwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali” alisema.
Akimzungumzia baba yake alisema marehemu alikuwa ni mtu ambaye anapenda utu ambapo alipenda kila binadamu ni sawa na hapaswi kubaguliwa.
Alisema wameamaua kumzika baba yao Dar es Salaam na si Mtwara kutokana na mke na mama yake kuzikwa Dar es Salaamna ndio utaratibu waliouweka wa kuzikwa.
“Baba alitaka kila mtu ambaye atafariki ni vyema akazikiwa hapo kwani hata wakati wa kulimia makaburi inakuwa rahisi,”alisema.
Kwa upande wake mtoto wa pili wa Marehemu Hilda Makaidi alisema baba yao alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.
“Nakumbuka nilimpigia baba simu akiniambia mwanangu Hilda Masasi kugumu, na mimi nikamwambia baba rudi nyumbani tukutibu lakini hakukubali haraka,”alisema.
Alisema baba ameacha mjane na watoto 10 huku ikiwa wakike wakiwa wanne na wakiume sita na wajukuu 10 na vitukuu sita.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi George Kahangwa alisema mazishi hayo yatahuduliwa na mgombea urais wa umoja huo Edward Lowassa  pamoja na viongozi wa taifa wa serikali na vyama vya siasa na vyama vya michezo.

“Sote tushiriki kumpa heshima za mwisho na kumsindikiza mpendwa wetu katika safari ya mwisho,”alisema.
Shughuli za kuuaga Mwilli wa Dkt.Emmanuel Makaidi zinaendelea katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam huku viongozi mbali mbali wakiwemo Mgombea urais wa Chadema na UKAWA,Edward Lowassa na Mgombea mweza Duni Juma Haji viongozi wa Serikali,Vyama vya siasa wakihudhuria.
Kufuatia kuagwa kwa Dkt.Makaidi Vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA vimelazimika kusitisha kampeni zake ili kushiriki mazishi hayo.

Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema kuwa lengo la UKAWA kusimamisha kampeni zao ni kumpa heshima marehemu (Dkt.Makaidi).
Marehemu aliacha wosia kuwa akifariki azikwe jijini Dar es Salaam ambapo mama yake na mkewe wa kwanza walikozikwa hivyo mwili wake ulisafirishwa kutoka Masasi mkoani Lindi.Alisema Makene.
 Dkt.Makaidi ni Miongoni mwa wagombea sita wa ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu waliofariki dunia na kusababisha uchaguzi wa majimbo kusimama.
Wagombea wengine waliofariki ni Mohamed Mtoi,Jimbo la Lushoto(CHADEMA),Celina Kombani,Jimbo la Ulanga Mashariki(CCM),Estomihi Mallah(Arusha Mjini,(ACT),Dkt.Abdallah Kigoda(Handeni -CCM,Deogratias Filikunjombe(Ludewa - CCM) 
Dkt.Emmanuel Makaidi alikuwa ni Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo wa UKAWA,Maziko yake yatafanyika kuanzia saa 8:30 mchana kwenye makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...