Friday, 16 October 2015

Mchague Maalim Seif, Chagua CUF aqngalia wananchi wampa sifa


Mchague Maalim Seif, Chagua CUF
Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na ukame wa kiongozi ambaye atajali matatizo yanayowakabili wananchi wake kwa kuyatafutia ufumbuzi. Wananchi wengi wa Zanzibar wamekuwa wakilalamika kila uchao juu ya Serikali yao kuwa ni yenye kuwadharau hatua iliyopelekea Serikali hiyo kushindwa kuleta majibu chanya kwa kero za wananchi hao.Licha ya matatizo hayo yanayowakabili Wazanzibari waliowengi kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji yao ya lazima ikiwemo Chakula, Malazi na Mavazi, Viongozi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi wao wanaendelea kujinufaisha wao na familia zao kwa kutumia jasho la Wananchi hao wanyonge.Oktoba 25 mwezi huu, ndiyo wakati muafaka wa kuuondoa utawala wa kidhalimu unaoongozwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kumchagua kwa kura nyingi Maalim Seif Sharif Hamad kutoka Chama Cha Wananchi CUF ili aweze kuyatatua matatizo hayo kwa kutuletea Mamlaka Kamili na Neema Kwa Wote.#MwakaWaMaamuziTwende na Maalim Seif Sharif Hamad: Rais wa Watu, Chaguo la WatuKwa #MamlakaKamili na #NeemaKwaWote
Posted by CUF Ushindi 2015 on Wednesday, October 7, 2015

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...