* NAMNA YA KUKUNJA KARATASI YA KUPIGA KURA (ballot Paper) BAADA YA KUPIGA KURA YAKO.
Utapewa karatasi ambayo itakuwa na majina ya wagombea.
Karatasi itakuwa na muonekano wa umbo la mstatili.
Inaweza kutokea kwa bahati mbaya baada ya kupiga kura kwenye nafasi ya mgombea uliyemchagua, ile kalamu uliyetumia ikawa inavuja wino.
Kuvuja wino kukasababisha kuathiri kura yako na ikaharibika wakati Wa ukunjaji karatasi hiyo.
Wakati wa kukunja karatasi yako ya kura ikunje kwa namna ifuatayo.
ishike karatasi ikiwa katika umbo la mstatili ikunje kwenda chini ili kuzuia wino kutoathiri mgombea mwingine na kura kuharibika, kwa kuikunja kwa namna hiyo hata kama wino unavuja utabaki katika sehemu ya mgombea uliyemchagua na kura yako itakuwa salama salimini.
Akihutubia Sengerema akiwa na Lowassa, mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameonyesha jinsi ya kupiga kura.
Kwanza kahadharisha kwamba usiamini kalamu ya Tume. Mimi sasa hivi ninaenda kununua BIC ishirini. Anasema siku ile ingia kwenye chumba cha kupigia kura kwa upole.
Ukishafika kwenye chumba cha kupigia kura, soma nenda kwenye orodha namba nne, utakuta picha Magufuli UNAACHANA NAYO kisha inayofuata ni ya Edward Lowassa na picha ya Duni kisha picha ya alama ya V ya CHADEMA. Mbele ya alama ya CHADEMA kuna kisanduku kiko wazi. Weka alama yako ya V na utakuwa umemaliza kupiga kura.
Kuhusu kukunja karatasi, unachotakiwa ni kuikunja kwa nje. Kukunja kwa nje kukoje. Barua ukiikunja huwa unakunja kwa kuficha maandishi. Lakini kukunja kwa nje ni kule kukunja ili maandishi yawe nje. Tena si yawe nje tu, bali mstari wa kukunja uwe kwa urefu yaani utoke juu kwenda chini.
Baada ya kukunja hivyo, karatasi itakuwa imejigawa mara mbili unayaona maandishi.
Sehemu ya tick uliyoweka, na sehemu ya yenye zile picha. Hapa unajiandaa na mkunjo wa mwisho. Mkunjo wa mwisho ni kwa kukunja kwa upana.
Ukumbuke ulipokunja tick ilikuwa upande wa kulia na ni ni vizuri ukawa uso kwa uso na zile tick baada ya kukunja. Kunjo la mwisho ni kwa upana unafanya hivi.
Huku zile tick ukiwa unaziona na picha ya Lowassa sasa imejificha, kunja kwa upana kwa maana ya kwamba tick inabaki nje.
Kwa kifupi ni kwamba unakuwa kama unaandika barua lakini karatasi imekuwa kama bahasha na unaitumbukiza pale posta huku anuani zinaonekana.
Narudia, ni ukunjaji ambao alama ya kura inakuwa kama anuani ya unakotuma barua.
Kama nimekosea mnisahihishe na mlioelewa zaidi tuhabarishane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured Post
Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...
-
Wakati umemualika mwanamke sehemu unayoishi ama wakati umetoka deti katika bar, unapaswa kujua ya kuwa kumsisimua mwanamke huanza kabla ya...
-
Na Baraka Mbolembole Wawakili waTanzania Bara katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, timu ya Yanga SC Jumamosi hii watakuwa na kib...
-
Mao alikuwa kiongozi Kichina Kikomunisti na mwanzilishi wa Jamhuri ya Watu wa China. Yeye alikuwa kuwajibika kwa sera za maafa ya ...
No comments:
Post a Comment