UKAWA wasimamisha Kampeni zao zote,kurejea Dar es salaam Kesho kumuaga MAKAIDI
Msemaji wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Bwana TUMAIN MAKENE |
Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umetangaza kusimamisha kwa kampeni zake kwa nchi nzima kwa siku ya kesho kwa ajili ya kumuaga na maziko ya aliyekuwa mwenyekitri mwenza wa umoja huo na mwenyekiti wa chama cha NLD Dk EMMANUEL MAKAID ambaye anataraji kuzikwa kesho jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Bwana TUMAIN MAKENE amesema kuwa Team zote za kampeni za umoja huo kesho zitalazimika kusimamisha kampeni na kurejea Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwenyekiti huyo aliyekuwa na mchango mkubwa katika umoja huo.
Mwenyekiti wa chama cha NLD Dk. Emmanuel Makaidi enzi za uhai wake |
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mwili wa Marehemu MAKAID utaagwa katika viwanja vya karimjee na baadae kuzikwa katika makaburi ya sinza Jijini Dar es salaam ambapo viongozi wakubwa wa vyama hivyo watashiriki akiwemo pia Mgombea urais wa Umoja huo Mh Edward Lowasa na viongozi wengine kutoka serikalini na Taasisi mbalimbali
No comments:
Post a Comment