Thursday, 16 March 2017

TRA YAFUNGA OFISI ZA TFF, WAFANYAKAZI WATOLEWA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) limezifungia Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

TRA kupitia Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart imewataka wafanyazi kuacha kila kitu cha shirikisho hilo ndani.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amethibitisha hilo na kusema TFF haikutimiza walichokubaliana kuhusiana na wanachowadai.

“Ni kweli tumezifunga na hiyo ni hatua ya mwisho kwetu kufanya hivyo. Tulikubaliana kulipa tunachowadai na muda umepita,” alisema.

Alipouliuzwa kuhusiana na kiasi: “Haya ni masuala ya sisi na wenyewe.”


Yono walihusika katika kuzifunga ofisi hizo na kuwataka wafanyakazi wote kutotoka nje ya ofisi na kuacha kilakitu ndani.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...