Thursday, 14 December 2017

Simba wamtaka mtambo wa magoli wazidi kujipanga, dirisha dogo sasa ni zamu ya Kassim Khamis

Image result for Kassim Khamis mchezaji
 
Simba imekaribia kuinasa saini ya mshambuliaji wa Zanzibar Heroes Kassim Khamis ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye ufungaji
Klabu ya Simba, ipo mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Zanzibar Heroes Kassim Khamis, ambaye ameonyesha kiwango bora katika michuano ya Kombe la Chalenji ambayo inaendelea nchini Kenya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe  ameiambia Goal, kila kitu kinakwenda vizuri na wanatarajia kumalizana na mchezaji huyo muda wowote kuanzia leo.
"Tunataka kufukuzana na muda kwasababu dirisha linafungwa Ijumaa, kwahiyo tutahakikisha kesho baada ya mechi ya nusu fainali dhidi ya Uganda anasaini fomu za kuichezea Simba kuanzia ligi itakapoendelea na huo kuwa usajili wetu wa tatu baada ya Jonas Sakuwah na  Asante Kwasi,"amesema Hans Poppe.
Straika huyo anayeitumikia Klabu ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya, amecheza mechi mbili pekee kwenye mashindano hayo kabla ya kuumia na kukosa mechi mbili zingine. Katika mechi hizo alizocheza, amefunga mabao mawili dhidi ya Rwanda na Kilimanjaro Stars.
Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masud Djuma, amesema katika kufuatilia kwake michuano hiyo, katika wachezaji wazawa amevutiwa na Khamisi kutokana na uchezaji wake pamoja na ushirikiano na wenzake anapokuwa uwanjani.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...