Leo ni siku ya kwanza kikosi cha Simba
kimeendelea ikiwa ni baada ya kujua itacheza na nani katika michuano ya
Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Simba imepangwa kuanza na Gendamarie ya Djibouti ambayo si timu ngumu sana ingawa haitakiwi kudhauliwa.
Simba imeendelea kujifua kujiandaa na
Ligi Kuu Bara katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jeshi la
Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Simba imekuwa ikifanya mazoezi kwenye uwanja huo kuhakikisha kikosi chake kinakaa vizuri.
Kwa takribani wiki moja, kikosi cha Simba kipo chini ya Kocha Msaidizi Madoud Djuma raia wa Rwanda.
Kocha huyo amekuwa akitoa mazoezi
mbalimbali na zaidi ni yake ya kutaka wachezaji kuwa na wepesi pia ya
ufundi katika ufungaji na kuzua kulingana na hali halisi.
No comments:
Post a Comment