Timu za taifa za Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' na Tanzania Visiwani 'Zanzibar Heroes' kesho zitakutana uso kwa uso katika mchezo wa pili wa kundi A, ambao utafanyika kwenye uwanja wa Kenyatta, uliopo Machakos Kusini mwa Kenya.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kutokana na wachezaji wa timu hizo mbili kufahamiana vizuri kutokana na kukutana kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Wenyeji wa mchezo wa kesho Zanzibar wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa juu ya ndugu zao Kili Stars, kwa kujikusanyia pointi tatu baada ya ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Rwanda wakati wenzao Kili Stars, wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na pointi 1, waliyoipata baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Libya.
Kilimanjaro Stars wanalazimika kushinda mchezo huo ikiwa wanahitaji kuweka hai matumaini ya kudelea mbele vinginevyo matokeo ya tofauti kinyume na ushindi timu hiyo inaweza kuungana na Rwanda kujiandaa kurudi nyumbani.
Kocha wa Zanzibar Hemed Morocco, ameuzungumzia mchezo huo wa kesho kwa kusema utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa na hiyo inachangiwa na wachezaji wa pande zote mbili kujua vizuri kutokana na muingiliano uliopo kwenye ligi.
"Nimchezo mgumu na wenye ushindani kwasababu Kili Stars, hawapo tayari kupoteza mchezo baada ya kwenda sare na Libya lakini hata sisi tunataka kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwasababu kama tunashinda mchezo huo tutafikisha pointi sita ambazo zinatupa uhakika wa kucheza hatua inayofuata," amesema Morocco.
Kwaupande wake Ammy Ninje kocha wa Kili Stars, naye ameupa mchezo huo jina la vita kwasababu ndiyo unaoshikilia matumaini yao ya kucheza hatua inayofuata ya michuano hiyo ambayo inafikia tamati Desemba 17 mwaka huu.
"Ukweli tumefanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya mchezo wa kesho natambua kuwa ni mgumu lakini kitu kizuri mimi na wachezaji wangu tumewaona Zanzibar wakicheza tumeona mapungufu yao na uzuri wao naamini tutajipanga kuhakikisha tunatumia madhaifu yao kuwafunga na kujiwekea uhakika wa kucheza hatua inayofuata,"amesema Ninje.
Katika kikosi chake cha kesho Ninje atamkosa mshambuliaji Mbaraka Yusufu ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja hivyo jukumu la ufungaji niwazi litabaki mikononi mwa Elias Maguri na Ibrahim Ajibu ambao ndiyo wanaonekana kuwa moto kwasasa.
Vita kali katika mchezo huo inatarajiwa kuwa kwenye eneo la kiungo na beki ya kushoto ambapo Hajji Mwinyi na Gadiel Michael watakuwa na kazi ya kupandisha mashambulizi ya timu zao katika kusaidia kupata ushindi ikumbuke kuwa wachezaji hawa wote wawili wanaichezea klabu ya Yanga.
Vita nyingine ipo kwenye eneo la kiungo ambapo Mohamed Issa 'Banka' aliyeibuka mchezaji bora wa mechi iliyopita dhidi ya Rwanda na Mudathir Yahya nao watakuwa na kazi kubwa ya kupambana na Himid Mao na Mzamiru Yasini.
Pamoja na Tanzania Bara au Kili Stars kupewa na fasi kubwa ya ushindi katika mchezo huo kutokana na ubora wa wachezaji walioitwa kwenye kikosi chao lakini Zanzibar imekuwa na bahati kubwa ya kuifunga Tanzania Bara kwenye michuano hiyo kwahiyo nilazima kila upande upambane kuhakikisha wanapata kile walichokusudiaVita ya Tanzania Bara na Visiwani leo kesho itajidhirisha wazi pale timu za taifa za ' Tanzania 'Kili Stars na Zanzibar Heroes zitakapo pambana
Timu za taifa za Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' na Tanzania Visiwani 'Zanzibar Heroes' kesho zitakutana uso kwa uso katika mchezo wa pili wa kundi A, ambao utafanyika kwenye uwanja wa Kenyatta, uliopo Machakos Kusini mwa Kenya.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kutokana na wachezaji wa timu hizo mbili kufahamiana vizuri kutokana na kukutana kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Wenyeji wa mchezo wa kesho Zanzibar wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa juu ya ndugu zao Kili Stars, kwa kujikusanyia pointi tatu baada ya ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Rwanda wakati wenzao Kili Stars, wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na pointi 1, waliyoipata baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Libya.
Kilimanjaro Stars wanalazimika kushinda mchezo huo ikiwa wanahitaji kuweka hai matumaini ya kudelea mbele vinginevyo matokeo ya tofauti kinyume na ushindi timu hiyo inaweza kuungana na Rwanda kujiandaa kurudi nyumbani.
Kocha wa Zanzibar Hemed Morocco, ameuzungumzia mchezo huo wa kesho kwa kusema utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa na hiyo inachangiwa na wachezaji wa pande zote mbili kujua vizuri kutokana na muingiliano uliopo kwenye ligi.
"Nimchezo mgumu na wenye ushindani kwasababu Kili Stars, hawapo tayari kupoteza mchezo baada ya kwenda sare na Libya lakini hata sisi tunataka kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwasababu kama tunashinda mchezo huo tutafikisha pointi sita ambazo zinatupa uhakika wa kucheza hatua inayofuata," amesema Morocco.
Kwaupande wake Ammy Ninje kocha wa Kili Stars, naye ameupa mchezo huo jina la vita kwasababu ndiyo unaoshikilia matumaini yao ya kucheza hatua inayofuata ya michuano hiyo ambayo inafikia tamati Desemba 17 mwaka huu.
"Ukweli tumefanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya mchezo wa kesho natambua kuwa ni mgumu lakini kitu kizuri mimi na wachezaji wangu tumewaona Zanzibar wakicheza tumeona mapungufu yao na uzuri wao naamini tutajipanga kuhakikisha tunatumia madhaifu yao kuwafunga na kujiwekea uhakika wa kucheza hatua inayofuata,"amesema Ninje.
Katika kikosi chake cha kesho Ninje atamkosa mshambuliaji Mbaraka Yusufu ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja hivyo jukumu la ufungaji niwazi litabaki mikononi mwa Elias Maguri na Ibrahim Ajibu ambao ndiyo wanaonekana kuwa moto kwasasa.
Vita kali katika mchezo huo inatarajiwa kuwa kwenye eneo la kiungo na beki ya kushoto ambapo Hajji Mwinyi na Gadiel Michael watakuwa na kazi ya kupandisha mashambulizi ya timu zao katika kusaidia kupata ushindi ikumbuke kuwa wachezaji hawa wote wawili wanaichezea klabu ya Yanga.
Vita nyingine ipo kwenye eneo la kiungo ambapo Mohamed Issa 'Banka' aliyeibuka mchezaji bora wa mechi iliyopita dhidi ya Rwanda na Mudathir Yahya nao watakuwa na kazi kubwa ya kupambana na Himid Mao na Mzamiru Yasini.
Pamoja na Tanzania Bara au Kili Stars kupewa na fasi kubwa ya ushindi katika mchezo huo kutokana na ubora wa wachezaji walioitwa kwenye kikosi chao lakini Zanzibar imekuwa na bahati kubwa ya kuifunga Tanzania Bara kwenye michuano hiyo kwahiyo nilazima kila upande upambane kuhakikisha wanapata kile walichokusudia..
No comments:
Post a Comment