LEO KATIKA HISTORIA
AFRIKA KUSINI WENYEJI WAKE NI KINA NANI HASA, UJIO WAO NA UBAGUZI.
Kama umekuwa ukifuatilia habari za kimataifa basi utakuwa umekutana na wanaojiita wenyeji Wa Afrika kusini kuwafukuza waafrika wenzao kwa kuwaita ni wageni.
Kabla hata hatujasahau machungu ya apartheid kule Afrika kusini tayari ile mbegu imeanza kuchipua tena na sasa si ubaguzi Wa mzungu na mwafrika bali ni ubaguzi Wa mwafrika na mwafrika mwenzake.
Cha kushangaza wamefikia hadi hatua ya kuua hadi watoto ilimradi tu ni mtoto Wa mgeni. Wanachokilalamikia hawa wanaojiita wenyeji ni kuwa eti wageni wamechukua ajira zao hivyo warudi nchini mwao ili nao wapate ajira hapa ndio Kiwango cha mwisho cha akili zao kufikiri.
NANI HASA MWENYEJI WA AFRIKA KUSINI.
Wenyeji Wa asili kabisa Wa Taifa la Africa kusini ni jamii za aina mbili. Jamii hizo ni SAN na KHOIKHOI. Jamii hizi zinafanana kwa kila kitu isipokuwa utofauti wao unaonekana kwenye shughuli wanazofanya ambapo San wao ni wawindaji na Khoikhoi ni wafugaji (refer peopling of south Africa)
Miaka 1000 kabla ya kristu kuzaliwa jamii ya WABANTU ilifika Africa kusini kama ambavyo walifika maeneo mengine ikiwemo hapa Tanzania na Kusini mwa sahara yote.
Walipofika Africa kusini walianza kuishi eneo la kwa Zulu Natal na baadaye kusambaa Afrika kusini yote na leo wanajiita Wenyeji Wa Africa kusini.
KUDHOOFIKA KWA WENYEJI WA ASILI.
Mwaka 1488 taifa la kwanza kutoka ulaya lilibisha hodi Afrika kusini. Taifa hilo ni taifa la Ureno. Ni mwaka huo ambapo Bartolomeo Diaz akiwa na wenzake walikuwa wakitafuta njia ya kuelekea bara Hindi kwa kupitia Atlantic halafu bahari Hindi mpaka India.
Safari yao ilianzia Mto Tagur uliopo Lisbon wakiwa njiani eneo la Angra ambapo sasa panaitwa Luderitzbutch Namibia walipigwa na dhoruba kali sana na kupoteza mwelekeo kwa muda mrefu.
Kwa bahati tu walitokezea mahali ambapo palikuwa na Rasi na Bartolomeo akapabatiza kwa kireno kwa jina la " cabo termentos" maana yake kwa kiingereza ni cape Strom yaani cape ya dhoruba.
Baadaye mreno mwenzake akatoa wazo la kupabadilisha jina na akapaita kwa kireno " Cabo da boa Esperenza" yaani Rasi ya Tumaini jema. Alipabadilisha jina kwa kuwa kwanza walipata matumaini ya kiendelea kuishi baada ya dhoruba baharini lakini pia walipata tumaini la kufika India kupitia hapo.
Hawa ni wareno Wa mwanzo kabisa kutia nanga na kukanyaga ardhi ya Africa kusini. Wakati hayo yakiendelea Wasan na wakhoikhoi wanashuhudia na walikuwa wakiendelea na shughuli zao kwenye mwambao huo Wa bahari.
Mwaka 1652 kampuni la " Dutch East Indias Company" walimtuma Jan van Reabeck akaweke ngome pale Afrika kusini. Ngome hiyo ingetumika kama station ya mabaharia Wa kampuni lao wakiwa wanaelekea India ikiwa ni pamoja na kupata vyakula vya njiani. Na mojawapo ya masharti aliyopewa ni kulima mbogamboga ili mabaharia wazipitie na kuzitumia njiani.
Kufika tu kwa Reabeck maisha ya wakazi Wa asili yalianza kubadilika. Waliongozana na Reabeck walianza kuwapora ardhi na kuwaibia mifugo yao. Wasan na wakhoikhoi hawakukubali na 1659 wakaamua kuanzisha vita.
Baadaye walilikimbia eneo lile na kuingia ndani zaidi ya Africa kusini. Kwa sasa hawa wajamaa wamejikita maeneo ya Kalahari. Huo ndio mwanzo Wa wenyeji kuondoka kwenye Ardhi yao ya asili.
Sasa tujiulize hawa wanaojiita wenyeji Wa Africa kusini wamesahau wslikotokea? Sitaki kuongelea zaidi kilichotokea Afrika kusini hadi kutawaliwa ila nadhani hawapo sahihi kwa kile wanachokifanya.

No comments:
Post a Comment