Friday, 26 January 2018

vanessa mdee asema amejitoa muhanga

Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amesema amejisikia faraja kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki albamu japokuwa anahisi amejitoa muhanga kwa maana hafahamu kama itakuja kumlipa.
Vanessa amebainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya muda mchache kupita tokea alipomaliza kufanya mapitio ya albamu yake iliyopewa jina la 'Money Monday' na kusema amesikia kelele nyingi kwa baadhi ya wasanii kwamba albamu bongo haiuzi.

"Nimefanya 'research' kwa muda mrefu sana na nimekugundua kwamba hakuna mfumo unao-support mauzo ya albamu lakini nikasema kama ninataka kukamilika kama msanii huko ninapoelekea na vitu ninavyotegemea kufanya sitaweza kuvikamilisha bila ya kuwa na 'CV' ya kusema kwamba nami nina albamu", alisema Vanessa.

Pamoja na hayo Vanessa ameendelea kwa kusema "mwisho wa mwaka huu 2018 nategemea kuachia nyingine jumla nitakuwa nazo mbili 'so' sijaweka uoga mbele nimeweka vitendaji kazi, 'i want people to see' nina uwezo wa kufanya vitu vingi na nimefanya 'risk'kwa sababu bado sijajua kama itanilipa lakini mpaka sasa hivi naona kama malipo yapo".

Kwa upande mwingine Vanessa amewashauri wasanii wenzake waache kusikiliza kelele za watu zinazodai kuwa albamu bongo hazifanyi vizuri huku akiwaomba mashabiki wake kuendelea kumpa ushirikiano wa kununua kazi yake hiyo ambayo inauzwa kwa njia ya mitandaoni na mkononi.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...