Friday, 19 January 2018

drogba ajenga shule nchini kwao


Mwanasoka Didier Drogba, mwenye asilia ya Ivory Coast, amefungua shule ya kwanza ya msingi , na kutangazwa leo.
Shule hiyo inatarajiwa kuwasaidia maelfu ya watoto walioko vijijini kwenye mashamba ya kakao ya jamii jamii ya Pokou-Kouamekro kupata elimu bora imearifiwa.
Katika sherehe za ufunguzi wa shule hiyo, Drogba alisema, tumeshughulika na mradi huu kwa miaka miwili na ninayo fahari kuona umekamilika.
Imani ya shirika langu daima imekuwa mara zote watoto wakipata fursa ya kupata elimu bora na huduma za afya zilizo bora, tutajenga kizazi chenye madaktari, wanasayansi, wafanya biashara wa kiume na wa kike na ndivyo tutakavyo ijenga Afrika iliyo bora zaidi.
Shule hiyo imejengwa chini ya ufadhili wa shirika la Didier Drogba, kwa ushirikiano mkubwa na kampuni ya Nestlé na mpango wa kimataifa wa uimarishaji zao la kakao .
Shule hiyo ina idadi ya vyumba vya madarasa sita, darasa la awali, kantini , maliwato, uwanja wa soka na nyumba za waalimu watatu. 

Arsenal wenger adaiwa kuitusi klabu ya Borussia

Mkufunzi wa Arsenal Arsene WengerMkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ''alitukosea heshima'' kwa kuzungumza hadharani kuhusu mchezaji Pierre-Emerick Aubameyang, amesema mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorc.
Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Gabon kwa dau la £60m.
Siku ya Alhamisi , Wenger alisema kuwa Aubameyang atafaa sana Arsenal , matamshi ambayo hayakuifurahisha klabu ya Dortmund.
''Tunahisi kwamba ni kukosa heshima kwa Wenger kuzungumzia kuhusu wachezaji wa klabu nyengine'', alisema Zorc.
''Hatujawasiliana na Arsenal''.
''Kwa sasa Arsene Wenger ana maswala mengi yanayompa changamoto ikiwemo mchezo wa wachezaji wake''.
Pierre-Emerick Aubameyang
Aubameyang ameadhibiwa mara mbili kwa utovu wa nidhamu msimu huu.

TUNZA NGOZI YAKO, EPUKA MATUMIZI MABAYA YA STEROIDI ZA KUPAKA.


Dawa za kupaka zenye steroidi ni zile zenye kutibu magonjwa ya ngozi kukakamaa na kuwa kavu (kwa kitaalam eczema), pia aina nyinginezo za magonjwa ya ngozi yasiyo ya uambukizi. Kama zilivyo dawa nyingine ambazo tunatumia kwa kumeza, dawa hizi za kupaka zenye steroidi huwa na maudhi ya dawa, pia madhara yasiyovumilika zinapotumika vibaya.

Dawa zenye steroidi za kupaka zaweza kugawanywa katika makundi makuu saba, kulingana na uwezo wa ufanyaji kazi wake. Na msingi mkuu wa matumizi ni kutumia kundi lenye uwezo wa chini kadri iwezekanavyo kwa jinsi itakayomfaa mgonjwa.

Kundi la I-Zenye uwezo wa juu kabisa.
Bethamethasone dipropionate.
Halobetasol propionate.
Clobetasol propionate.

Kundi la II-Zenye uwezo wa juu.
Mometasone furoate
Desoximetasone

Kundi la III, IV, V  na VI-Zenye uwezo wa kati
Fluticasone propionate
Triamcinolone acetonide
Desonide
 Fluocinolone acetonide
Kundi la VII-Zenye uwezo wa chini
Hydrocortisone
Kumekuwa na wimbi la matumizi ya dawa za kupaka zenye steroidi miongoni mwa wanajamii bila ya kupata ushauri wa wataalamu wa ngozi.Wengi wa watumiaji huzitumia kama vipodozi. Wahanga wakubwa ni wanawake ingawa na wanaume pia wamekuwa wakijihusisha na matumizi mabaya ya dawa hizi. Madhara wapatayo watu hawa wanaotumia dawa hizi zenye steroidi za kupaka kiholela, ni wazi kwa muonekano wa ngozi zao. Pia kuna madhara mengineyo mengi ndani ya mwili ambayo mtumiaji holela anaweza kupata, hii ni kwa sababu dawa hizi pia zina uwezo wa kusharabiwa mwilini.

Dawa hizi za kupaka zenye steroidi huwa hazina madhara endapo mtumiaji atatumia kama alivyoandikiwa na daktari wa ngozi, chini ya uangalizi na ufuatiliaji wa watataalamu wa afya. Dawa hizi za kupaka kwa mfano ni kama Dermovate®, Diprosone®,Sonaderm®,Gentrisone®,Safi®,Elyvate®,Betason®, Betacort® na nyinginezo nyingi.

Dawa za kupaka  zenye steroidi husharabiwa mwilini na kuingia katika damu, na kiasi kinachosharabiwa hutegemea na ukubwa wa eneo la ngozi mtu anapaka na kiasi cha dawa anachopaka kwenye ngozi. Zile zenye uwezo wa chini husharabiwa katika maeneo mengine ya ngozi isipokuwa kiganja, lakini zile zenye uwezo wa juu husharabiwa kwenye ngozi na pia katika kiganja. Kiasi kikubwa cha dawa husharabiwa zaidi katika maeneo ambayo ngozi ni nyembamba, mfano karibu na macho, sehemu za siri na sehemu za mikunjo ya ngozi.


Madhara katika ngozi yanayosababishwa na utumiaji holela wa steroidi za kupaka yatategemea na kiasi anachopaka mtumiaji na uwezo wa steroidi anayopaka, lakini madhara haya kwa ujumla ni kama ifuatavyo; kupungua kwa kinga ya ngozi, ambapo itapelekea mtumiaji kupata uambukizi wa fangasi hata bakteria katika ngozi kwa urahisi, na kwa uchache pia malengelenge na hata mkanda wa jeshi. Husababisha matatizo  kama chunusi na ukavu wa ngozi. Ngozi kuwa nyembamba ambayo hupelekea michiri, ngozi kuchubuka kwa urahisi, rashezi kuzunguka mdomo, kupoteza nywele na kuungua jua kwa urahisi. Kutanuka kwa mishipa ya damu, ambayo husababisha kuonekana kwa mishipa ya damu katika ngozi,pia wekundu katika ngozi huonekana mtumiaji anapoacha kutumia.

Dawa hizi zaweza kuleta madhara mwilini endapo zitatumika kiholela.Kiasi kikubwa cha dawa za kupaka zenye steroidi,mojawapo au zaidi kutoka makundi ya steroidi,  husharabiwa katika kiwango ambacho huathiri kazi za tezi ya adrena. Tezi hii inahusika na utengenezaji wa steroidi za asili mwilini, ambazo ni muhimu katika kuiweka miili yetu katika afya njema . Steroidi hizi katika dawa za kupaka zinaposharabiwa na kuwepo mwilini, mrejesho wa taarifa kutoka katika ubongo hupelekwa katika tezi ya adrena, na tezi hii huacha kutengeneza steroidi za asili. Endapo mtumiaji ataendelea kutumia dawa hizi kwa muda mrefu, tezi hii husinyaa kwa kuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu. Endapo mtumiaji ataacha kwa ghafla matumizi ya steroidi hii atakuwa mgonjwa na udhaifu wa mwili utakuwa dhahiri,na endapo ataendeleza matumizi ndivyo atazidi kuathirika kadri siku zinavyosonga. Madhara atakayopata mtumiaji holela endapo kiasi kikubwa kitasharabiwa ni ugonjwa ujulikanao kama Cushing syndrome, dalili za ungonjwa ni uso wa mviringo, kuota nundu ya mafuta kati ya mabega.Alama za michirizi katika ngozi ambazo husababishwa na ngozi kuwa nyembamba na kutanuka, au kutanuka kwa mishipa ya damu . Pia kukusanyika kwa maji mwilini(edema), shinikizo la juu la damu, udhaifu wa mifupa na mara chache pia kisukari. Matibabu ya ugonjwa ni uangalizi wa karibu na jinsi ya kumwachisha mgonjwa matumizi ya steroidi, ili kurejesha mfumo wa asili.Matibabu huwa na mafanikio endapo mtumiaji atawahi kutibiwa.

Steroidi katika dawa hizi husharabiwa na kupita placenta. Kwa hiyo mama mjamzito awe makini na kupata ushauri wa daktari. Steroidi pia hutolewa katika maziwa ya mama anayenyonyesha. Uangalizi maalumu huhitajika endapo mama anayenyonyesha atakua anatumia dawa hizi. Kwa watoto, steroidi huathiri ukuaji wa mtoto, kwa hiyo watoto ni kundi ambalo pia huhitaji ungalizi maalumu katika matumizi haya ya dawa za steroidi za kupaka.

Kuna vipodozi vyenye steroidi ambavyo huuzwa kinyume cha sheria, steroidi hizi katika vipodozi hivi hupatikana katika makundi ya steroidi tuliyoyaona awali. Madhara yake ni sawa pia kama tulivyoyaona hapo awali.Kipodozi maarufu ambacho hutumika sana na kinamama ni Caro®light (kipodozi kilichopigwa marufuku). Chukua tahadhari endapo unaamua kubadilisha aina ya kipodozi. Wasiliana na mfamasia au mtaalamu wa ngozi endapo una mashaka na aina mpya ya kipodozi unachotaka kutumia.

Endapo wewe ni mtumiaji holela wa dawa za kupaka zenye steroidi, wahi haraka hospitali au kwa daktari wa ngozi kwa ajili ya ushauri na matibu. Wasiliana na mfamasia wako kwa ushauri juu ya matumizi bora ya dawa za kupaka zenye steroidi. Kamwe usichukue maamuzi mwenyewe, usishawishiwe na rafiki au ndugu kutumia dawa hizi zenye steroidi pasi na ushauri wa daktari wa ngozi. Hakikisha umeelewa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa kwa kuuliza maswali.

Dawa za kupaka zenye steroidi ni zile ambazo mtumiaji hutumia kwa kuandikiwa na daktari, na siyo kununua na kutumia bila kumwona mtaalamu wa ngozi.

Mama Aliyesemekana Amejifungua KOPO


IVORY COAST 0- 2 ZAMBIA

#CHAN2018 Mpira umekwisha, Zambia yatinga hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo.

FT'- Ivory Coast 0-2 Zambia
Itakapotimu saa 4:30 itakuwa zamu ya Uganda dhidi ya Namibia. Burudani hiyo italetwa kwako mbashara kupitia #ZBC2

wanaigeria wapaniki kisa tuzo ya Daimond platnumz ya soundcity

Wanigeria wamvimbia Diamond Platnumz kisa tuzo ya SoundcityMVPBaada ya msanii wa muziki Diamond Platnumz kutoka Tanzania, kuibuka msindi wa tuzo ya muziki ya Soundcity MVP Awards 2017, kupitia kupengere cha ‘Best Male MVP’ wadau na mashabiki wa muziki nchini Nigeria wameonyesha kutofurahishwa na ushindi huo.


Katika kipengere hicho alichoshinda Diamond, alikuwa akichuana na wasanii kama Runtown, Davido, Olamide, 2face Idibia, Wizkid, Shatta Wale, Navio na Sarkodie.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter mashabiki hao wameonyesha hisia zao za kutofurahia ushindi wa msanii huyo.

7h

Osas Cruz
@OsasCruz
Replying to @OsasCruz
Davido Giving Shout-out to Wizkid acknowledging his hard work. That's how it should be #SoundcityMVP 👏 pic.twitter.com/Igugtebz19


Osas Cruz
@OsasCruz
How Diamond Platnumz beat Wizkid, Davido, Olamide, to win the BEST MALE MVP should be the greatest fraud ever 😎

9:30 AM - Jan 13, 2018
 8 8 Replies   24 24 Retweets   84 84 likes
Twitter Ads info and privacy

Övie

@OvieO
Diamond who???!!!!! Best Male??!!! This place just flipped!!! Hooooowwww????!!!!!

2:50 AM - Jan 13, 2018
 9 9 Replies   25 25 Retweets   24 24 likes
Twitter Ads info and privacy
View image on Twitter
View image on Twitter

pls follow back®
@Slyxra
Best male Diamond platnumz... Wait how

3:38 AM - Jan 13, 2018
 4 4 Replies   29 29 Retweets   44 44 likes
Twitter Ads info and privacy
13h

SOUNDCITY AFRICA!

@SOUNDCITYtv
Diamond Platnumz wins 'Best Male Act' at the #SoundcityMVP!

Stream Live on: http://soundcity.tv/themvp-liveblog


Lil iz
@LilizMusic
pls

mention just one hit single from diamond that took AFRICAN AIR IN 2017 @SoundcityMVP 

diamond ko BRONZE NI#SoundcityMVP

3:11 AM - Jan 13, 2018
 7 7 Replies   Retweets   8 8 likes
Twitter Ads info and privacy
13h

SOUNDCITY AFRICA!

@SOUNDCITYtv
Diamond Platnumz wins 'Best Male Act' at the #SoundcityMVP!

Stream Live on: http://soundcity.tv/themvp-liveblog


Scrappi
@Scrapp_i
You people should not do and end up like “HEADIES AWARD” what’s diamond platnumz, stop joking with us and give us the real winner pic.twitter.com/3RBAf7tovf

4:58 AM - Jan 13, 2018
View image on Twitter
 Replies   Retweets   1 1 like
Twitter Ads info and privacy
Ugawaji wa tuzo hizo umefanyika usiku wa jana nchini Nigeria na msanii Davido aliibuka kinara kwa kutwaa tuzo tatu kubwa ambazo ni ‘Song of the Yeara’, Video of the year’ na ‘African Artist of the Year Award’. 

wakili asema kufanya ukahaba sio kosa kisheria

Image result for prostitution in tanzaniaBiashara ya Ukahaba ni miongoni mwa biashara zinazopigwa vita duniani, ambapo leo January 18, 2018 wakili wa kujitegemea Juma Nassoro amesema kisheria ni kosa kufanya Ukahaba kwa ajili ya kujipatia kipato.

 Akizungumza na AyoTV, Wakili Nassoro amesema kuwa kisheria kufanya Ukahaba si kosa, isipokuwa kufanya Ukahaba kwa lengo la kibiashara ni kosa.

“Kidini ukahaba ni makosa lakini kwa sheria za nchi yetu mtu kuwa na mahusiano na watu tofauti tofauti sio kosa, isipokuwa litakuwa kosa la kijinai ni kufanya kazi hiyo kwa kujiingizia kipato na endapo akitiwa hatiani adhabu yake ni kifungo ama faini,”.– Wakili Juma Nassoro

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...