Takriban maafisa 63 wa kikosi cha polisi nchini Kenya wamefutwa kazi kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.
Msemaji wa polisi ni miongoni mwa wale waliofutwa kazi kulingana na mwandishi wa BBC Joseph Odhiambo.
Tume ya huduma za maafisa wa polisi iliwafuta kazi maafisa hao baada ya kuwakagua maafisa 1,300 kwa kipindi cha miezi 14.
Mbali na msemaji wa kikosi cha polisi wa utawala Masoud Mwinyi,wengi wa wale waliosimamishwa kazi wanatoka katika idara ya trafiki.
Mwenyekiti wa tume hiyo Johnston Kavuludi amesema kuwa wakati wa ukaguzi huo waligundua kwamba maafisa wa vyeo vya chini wanaofanya kazi katika idara hiyo walikuwa wakituma kiwango cha fedha wanachopata kwa maafisa wanaowasimamia kupitia simu zao.
bbc swahili
No comments:
Post a Comment