Thursday, 7 December 2017

Bendera ameacha rekodi inayotesa makocha

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Joel Nkaya Bendera amefariki dunia jioni ya December 6, 2017 katika hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya kifo cha Joel Bendera imethibitishwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha hospitali ya taifa Muhimbi Aminiel Eligaeshi: “Ni kweli tumempokea hospitalini kwetu majira ya 6:03 katika idara yetu ya magonjwa ya dharura akitokea hospitali ya Bagamoyo . toka alipofika madaktari wetu walikuwa wanafanya kazi ya ziada kuhakikisha wanaweza kuokoa maisha yake.”
“Waliendelea kuwepo pale idara ya magonjwa ya dharura hadi saa 10:24 alipoaga dunia, sisi kama hospitali haturuhusiwi kutaja ugonjwa wa mtu anapofariki, mwenye dhamana ya kufanya hivyo ni daktari na ndugu wa marehemu.”
Bendera amefariki huku rekodi yake ikiwa bado haijavunjwa ya kuiwezesha Taifa Stars kufuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria. Makocha wazalendo na wageni wengi tayari wameshapita lakini hakuna aliyeifikia rekodi hiyo iliyodumu kwa miaka 37.
Juma Pondamali ‘Mensa’ na Leodgar Tenga ni baadhi ya wachezaji ambao walikuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichoshiriki fainali za Afrika mwaka 1980, wawili hao bado wanaendelea kulitumikia soka katika nafasi tofauti.
Ukiachana na masuala ya soka, Bendera alikuwa ni mwanasiasa nguli nchini ambapo aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za uhai wake. Aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, pia aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na Manyara kwa nyakati tofauti.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...