Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amebainisha kuwa kiungo wake Santi Cazorla atakuwa nje hadi mwezi Februari na "ataanza sifuri" kufuatia upasuaji aliofanyiwa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania bado anauguza majeraha yake ya mguuni ambayo yamemweka nje tangu Oktoba 2016 na amefanyiwa oparesheni tisa tofauti kwa tatizo lake wiki iliyopita.
Wenger alitaraji kuwa mchezaji wake huyo mwenye umri wa miaka 32 angeweza kuanza kucheza 2018 lakini akiongea kabla ya mechi ya Europa ya Arsenal dhidi ya BATE Borisov,Mfaransa huyo amekiri kuwa majeraha mapya yanamaanisha kuwa anaweza kurejea angalau Februari.
"Kwa bahati mbaya anatakiwa kuanzia sifuri tena," alisema bosi wa Arsenal.
"Hii inamaanisha kuwa ikiwa ataendele vizuri hadi atakapoweza kukimbia na atakapoanza kukimbia itamchukua angalau wiki sita kurejea mazoezini. Lini ataweza tena kukimbia sijui."
Arsenal wataikabili BATE kwenye mechi ya Ligi ya Europa jioni ya leo, wakifahamu kuwa tayari wameshakamata nafasi ya kwanza Kundi H
No comments:
Post a Comment