Thursday, 14 December 2017

jokate awafunda vijana katika kutumia muda wao vizuri

Jokate ambaye ni mjasiliamali pamoja na mhamasishaji haswa kwa vijana, kwa sasa yupo katika kampeni ya kuwakumbusha vijana wajibu wao ili waweze kujitambua kupitia kampuni ya Sahara Group inayo saidia kuwapa Elimu vijana juu ya mustakabali wamaisha yao.
''Vijana wasitumie mitandao ya kijamii kujua kuwa Jokate amevaaje leo, au kaweka nywele gani , inatakiwa watafute taarifa mbalimbali ambazo kila wakati hutolewa katika 'Internet' ili ziweze kuwapa ufahamu na pengine kuwasaidia,'' amesema.
Pia Jokate ameendelea kuzungumza kwa kusema, ''Ni vizuri kijana kuwa na kazi yake akijiamulia mwenyewe kwamba leo afanye kazi gani na afanye nini anakuwa huru sana,'' ameongeza
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa njia sahihi ya elimu kwa vijana juu ya kujitegemea ianzie vyuoni ili wakati wanapomaliza wanakuwa tayari wameweza kujua njia sahihi ya kuji kwamua.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...