Headlines za Mbwana Samatta kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa michuano ya klabu Bingwa barani Afrika bado zinazidi kuchukua nafasi, baada ya November 11 kurejea Dar Es Salaam akitokea Lubumbashi Congo ambako ndio makao makuu ya klabu yake ya TP Mazembe ambayo Jumapili ya November 8 ilitwaa taji la klabu Bingwa Afrika kwa kuifunga klabu USM Alger ya Algeria kwa jumla ya goli 4-1.
Hizi ni pichaz za mapokezi ya Mbwana Samatta aliyoyapa kutoka kwa familia yake baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Dar Es Salaam, baada ya kurudi Tanzania Samatta atajiunga na kikosi cha Taifa Starsambacho kinarejea leo November 11 saa 12 jioni kutokea Afrika Kusini kilipokuwa kimeweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018Urusi. Taifa Stars itacheza na Algeria Jumamosi ya November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment